Vigezo na masharti

Updated: 16/01/2026

1.      KARATA 3 ni mchezo unaosimamiwa na Lucky games na kuthibitiwa chini ya Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (Tanzania Gaming board)

2.      Sheria na masharti yafuatayo yanatumika kwenye KARATA 3. Kwa kushiriki katika mchezo huu, utachukuliwa kuwa umesoma, umeelewa na umekubali vigezo na masharti

3.      Vigezo na masharti haya yanajumuisha makubaliano ya lazima kati yako na KARATA 3.

4.      KARATA 3 haki ya kurekebisha/kubadili vigezo na masharti muda wowote na bila ya taarifa ya awali. Ni jukumu lako kukagua/kuangalia makubaliano na marekebisho hayo kila wakati unapocheza, pamoja na sheria mahususi ya kila mchezo unaochagua kushiriki, ili kuwajibika na marekebisho yote.

5.      Unaelewa kikamilifu na unakubali kufungwa na vigezo na masharti yaliyomo na yanayoweza kurekebishwa nasi mara kwa mara.

6.      Kanuni na maelezo ya kisheria za kila mchezo zinazotolewa kivyake kwenye mchezo hujumuishwa katika kurejea vigezo na masharti.

Hati ya umiliki

1.      BENTER GROUP LIMITED ndiye mmiliki pekee wa chapa ya biashara ya KARATA 3 na nembo ya KARATA 3. Matumizi yoyote ambayo hayajaidhinishwa na nembo ya biashara ya KARATA 3 inaweza kusababisha kukufunguliwa mashtaka

2.      www.karata3.co.tz ni tovuti pekee ya KARATA 3 na hakuna matumizi yasiyoidhinishwa yanayoweza kufanywa ya URL hii kwenye tovuti nyingine au jukwaa la kidijitali bila idhini yetu ya maandishi

3.      BENTER GROUP LIMITED ndiye mmiliki au mwenye leseni halali ya haki za teknolojia, programu na mifumo ya biashara inayotumika ndani ya mfumo huu.

4.      Yaliyomo na muundo wa KARATA 3 iko chini ya hakimiliki © na haki za uhifadhi taarifa kwa jina la KARATA 3. Haki zote zimehifadhiwa. Hakimiliki katika mchezo huu ikijumuisha maandishi, michoro, msimbo, faili na viungo vyote ni vya KARATA 3 na tovuti haiwezi kunakiliwa, kupitishwa au kuhifadhiwa kwa sehemu bila idhini yetu ya maandishi. Usajili wako na utumiaji wa mfumo wetu haitoi haki yoyote ya kimiliki iliyo katika mfumo wetu.

5.      Links/viuongo katika mchezo huu haziwezi kujumuishwa kwenye tovuti nyingine yoyote bila kibali cha maandishi cha KARATA 3

6.      Unakubali kutotumia kifaa chochote kiotomatiki au cha mwongozo kufuatilia MCHEZO WA KARATA 3 au maudhui yoyote ndani yake. Matumizi yoyote ambayo hayajaidhinishwa au kuzaliana yanaweza kushtakiwa

Utatuzi wa migogoro

Mgogoro wowote utakaojitokeza baina ya pande mbili tajwa hapo juu utatatuliwa na Mahakama yenye mamlaka kwa kutumia sheria za JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ukiukaji, Adhabu na kutolewa kwenye huduma

1.      Iwapo Utakiuka kifungu chochote cha vigezo na masharti haya au KARATA 3 imeshuku ukuikwaji,KARATA 3 inayo haki ya kutofungua, kusimamisha, kufunga Akaunti yako ya ushiriki, kuzuia malipo ya ushindi wako na kutumia fedha hizo kwa sababu ya uharibifu wowote unaodaiwa na wewe

2.       Iwapo KARATA 3 inashuku kuwa unajihusisha na shughuli zisizo halali au za ulaghai unapotumia mchezo huu; au kukiuka makubaliano haya; au kwamba una matatizo na wakopeshaji au unadhuru biashara yetu, tunaweza kukufungia au kusimamisha akaunti yako kwa hiari yetu kabisa.

3.      Unakubali kwamba KARATA 3 ndiyo atakuwa mtoa maamuzi wa mwisho ikiwa umekiuka sheria, vigezo na masharti ya KARATA 3 kwa namna ambayo itasababisha kusimamishwa kwako au kuzuiwa kabisa kushiriki mchezo huu

Sera ya faragha

1.      Kwa hivyo unakubali kwamba ni muhimu kwa KARATA 3 kukusanya na kuchakata taarifa yako binafsi ili kukuwezesha na kukuruhusu kushiriki katika michezo. Taarifa yako binafsi iliyokusanywa itahifadhiwa na KARATA 3 hadi itakapohitajika kwa madhumuni ya kutoa huduma.

2.      KARATA 3 italinda taarifa zako binafsi na kuheshimu faragha yako kwa mujibu wa kanuni bora za biashara na sheria zinazotumika.

3.      KARATA 3 itatumia tu taarifa yako ya binafsi ili kukuruhusu kushiriki katika mchezo na kutekeleza shughuli zinazohusiana na ushiriki wako katika mchezo, na kwa madhumuni ya kutekeleza taratibu za uthibitishaji kuhusiana na ushiriki wako katika mchezo kama huu.

4.      Taarifa zako binafsi hazitafichuliwa kwa wahusika wengine, isipokuwa ufichuzi kama huo ni muhimu kwa ajili ya kushughulikia maombi yako kuhusiana na ushiriki wako katika michezo au isipokuwa kama inavyotakiwa na sheria. Kwa washirika wa biashara wa KARATA 3 au wasambazaji.

5.      Una haki ya kupata taarifa zako binafsi inayohifadhiwa na kushikiliwa na KARATA 3 kukuhusu wewe.

6.      Ili kukupa huduma bora, KARATA 3 na/au watoa huduma wake wanaweza kuhitaji kutoa taarifa yako binafsi kutoka kwa mshirika wa kibiashara mmoja hadi mwingine. Kwa hivyo unakubali taarifa yako ya binafsi ihamishwe hivyo

7.      Katika uchakataji wa akaunti yako ya ushirika na miamala inayohusiana nayo, KARATA 3 inaweza kuwa na njia ya kufichua taarifa kwa mashirika ya ukadiriaji wa mikopo, mashirika ya kugundua ulaghai na mashirika ya kupambana na ufujaji wa pesa. Kwa hivyo unakubali ufichuzi kama huo.

8.      Tunaweza pia kukujulisha kuhusu mabadiliko, huduma mpya na matangazo tunayofikiri kuwa yanaweza kukuvutia.

9.      KARATA 3 itapeleka taarifa zako za binafsi kwa Mamlaka husika katika Bodi ya kubashiri Tanzania inapolazimika kisheria kufanya hivyo, na haitawajibika kwa matokeo yoyote ambayo yanaweza kutokea kutokana na kutenda kwa mujibu wa sheria.

Mwisho
Imetolewa: 16/01/2026